Klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani imethibitisha kwamba kiungo wake Julian Draxler atajiunga na Paris Saint-Germain (PSG) baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo Januari mwakani.

Taarifa kutoka klabu hiyo imesema kuwa makubaliano yamefikiwa kwa timu zote mbili na kiungo huyo atasaini mkataba wa miaka minne na nusu kwa mabingwa hao wa Ufaransa atakapofaulu vipimo.

Mkuu wa michezo wa Wolfsburg, Olaf Rebbe amesema kuwa walikubaliana na kiungo huyo na kuamaua kujiunga na klabu hiyo ya Ufaransa.

Naye kocha wa klabu hiyo, Valerian Ismael amesema kuwa anajutia kuondoka kwa Julian Draxler kwasababu ni mchezaji mzuri lakini anafikiri hatua aliyoipiga ni nzuri kwa pande zote.

Draxler alijiunga na Wolfsburg akitokea klabu ya Schalke mwaka 2015 na ameshinda magoli matano katika mechi 34 za ligi ndani ya klabu hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *