JuKwaa la Wahariri nchini Tanzania (TEF) limevitaka vyombo vya habari nchini kutoandika au kutangaza habari zozote zinazomuhusu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na kuwalazimisha watangaza wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kinachomuhusu Askofu Gwajima.

Azimio hilo limetolea leo na Jukwaa hilo la Wahariri baada ya kufanya kikao leo jijini Dar es Salaam.

TEF pamoja na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu ikiwemo.

  1. Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda
  2. Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.
  3. Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *