Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limesema linajiandaa kuiwekea Sudan kusini vikwazo vya silaha, ikiwa itajaribu kuzuia kupelekwa kwa wanajeshi wa ziada wa kulinda amani nchini humo.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema hataruhusu Umoja wa Mataifa kuchukua udhibiti wa nchi yake na hatoshirikiana tena na umoja huo.

Kikosi hiko cha Umoja wa Mataifa kitakachoundwa na askari wa Afrika kitakuwa na majukumu makubwa zaidi ya askari zaidi ya 12,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wako tayari katika taifa hilo.

Mapigano baina ya vikosi hasimu ya mwezi Julai yaliwauwa mamia ya watu na wengine maelfu kadhaa kuyakimbia makazi yao.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinakabiliwa na kazi ngumu ya kuwalinda raia ambapo zaidi ya watu 35,000 walikimbilia kwenye makao makuu yake mjini Juba.

Tofauti na kikosi cha kulinda amani kilichopo nchini humo, kikosi cha Afrika kitakachokua chini ya Umoja wa Mataifa kitaweza kukabiliana na wale watakaowatishia raia

Hata hivyo haijawa wazi ikiwa kikosi hicho kitaweza kufanya kazi bila ushirikiano na Sudan kusini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *