Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuyafuta makampuni ya simu yatakayoshindwa kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua mfumo mpya wa ukusanyaji kodi kwa njia ya kielektroniki maeneo ya Kijitonyama.

Pia ameziagiza taasisi za Serikali na Kampuni binasfi kujiunga na mfumo wa ukusanyaji wa mapato ili kuiwezesha Serikali kupata kodi bila uonevu wowote.

Rais Magufuli pia amepiga marufuku wizara na taasisi nyingine Serikali kuanzisha vituo vya taarifa kwa kuwa vilivyopo vingi na vinatumia gharama kubwa wakati wa kuanzishwa.

Magufuli amesema kuwa mfumo huo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki unafaida yake hivyo amewataka wawekezaji na wafanyabiashara kukitumia chombo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *