Muigizaji wa vichekesho nchini kutoka kundi la Olijino Komedi, Joti ameuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake leo jijini Dar es Salaam.

Picha zilizosambaa mitandaoni zinamuonesha mchekeshaji huyo akiwa katika pozi mbali mbali kwenye harusi hiyo akiwa pamoja na mke wake huyo katika gari ya pamoja huku wakiwapungia mkono watu waliokusanyika barabarani.

Joti anafuata nyayo za mchekeshaji mwenzake Masanja Mkandamizaji ambaye amefunga ndoa mwaka jana.

Tazama picha za ndoa hiyo ilivyokuwa.

joti2

joti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *