Kocha wa Man United, Jose Mourinho amekanusha kuwa na mgogoro na mshambualiaji wa timu hiyo Anthony Martial baada ya mfaransa huyo kuonekana nyumbani kwao kwenye jiji la Paris mwishoni mwa wiki iliyopita wakati United ilipokuwa ugenini ikipambana na Stoke City.

Taarifa kutoka ndani ya United zinasema kuwa mchezaji huyo aliachwa nje ya kikosi hicho na alipewa ruhusa ya kupumzika.

Lakini wakati mechi ikiendelea ripoti zikaanza kuvuja kuwa mfaransa huyo alikuwa nyumbani kwao Ufaransa.

Hata hivyo Mourinho alipokuwa akizungumza kabla ya mechi ya marudiano ya kombe la EFL dhidi ya Hully City alisema kuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza wana michezo mingi ya kucheza huvyo huwapumzisha na kuwapa mzunguko unaowasaidia kulinda viwango vyao.

‘Hatuna siku nyingi za kupumzika hivyo huwa napenda kuwapa uhuru wachezaji ambao sijawachagua kwaajili ya mechio kuchagua iwapo wanataka kupumzika na kama yeye alichagua kwenda Parisi, hilo si tatizo kabisa’.

‘Endapo hadi kufikia mwisho wa juma hakutakuwa na majeruhi, nitamchezesha Romero hivyo David de Gea atakuwa huru na kama ataenda Hispania ni chaguo lake hivyo hakuna tatizo kabisa kwa Martial kwenda Paris’

Martial amekuwa akivumishwa na uhamisho wa mkopo kurudi Ufaransa lakini Mourinho ameweka wazi msimamo wake kuwa ingawa Martial bado hajawa kwenye kiwango bora lakini hatouzwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *