Mwanamitindo, Jokate Mwegelo maarufu kama ‘Kidoti’, amekutana  na aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Thierry Henry nchini Afrika Kusini.

Jokate ameweka picha katika akaunti yake ya Instagram akiwa na staa huyo wakiwa nchini Afrika Kusini kwenye mechi za mpira wa kikapu nchini humo.

 Kwa mujibu wa picha hizo zilizosambaa mitandaoni jana, wawili hao walikutana Johannesburg nchini Afrika Kusini katika Ligi ya Mpira wa Kikapu (NBA) ya Afrika kwa mwaka 2017.

Jokate ambaye ni Balozi wa NBA kwa upande wa Afrika alihuduria mashindano hayo yaliyokutanisha timu za NBA kwa wachezaji wenye asili ya Afrika na wale wa mataifa mengine.

Katika hali iliyoibua sintofahamu na maswali kibao, katika picha moja alionekana na mavazi tofauti na yale aliyoonekana nayo awali, lakini picha zote akiwa na Henry katika sehemu iliyosadikiwa kuwa ni hotelini huku wakionekana ni wenye furaha.

Jokate aliweka picha hizo na kuandika: “Nahamia Arsenal rasmi, naomba ushauri, lakini naambiwa Arsenal ni stress tupu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *