Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo (Kidoti) amesema kuwa atarudi kwenye muziki japokuwa yupo kimya kwasasa.

Kidoti amesema hayo baada ya mashabiki wake kumuona kimya kwenye muziki kwani amekaa muda mrefu bila kutoa nyimbo ikiwa tayari ana nyimbo zaidi ya tatu japo aliahidi  kurudi tena mwishoni mwa mwezi huu. 

Jokate amesema kuna mipango ambayo wanaiweka sawa hivyo mashabiki zake wasubiri kwani tayari ana nyimbo nyingi ambazo ameshazirekodi na akashindwa kuzitoa kutokana na kazi za kampuni yake ya kidoti kuwa nyingi.

 

Pia Jokate amesema anategemea kufanya kazi na waongozaji kutoka Kenya na Uganda kwa upande wa bongo movie na hiyo itakuwa siku za karibuni zaidi ikiwezekana mwanzoni mwa mwaka ujao.

 

Mwanamitindo huyo pia ni mjasiliamali wa kujitegemea kwani hivi juzi kupitia brand yake ya Kidoti ameingiza sokoni bidhaa za mabeki yanye nembo hiyo ya Kidoti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *