Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo leo ametoa misaada katika kituo cha kulelea watoto yatima  na wajane cha Ahbaabul Khairiya kilichopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Jokate ametoa mchele kilo 250, Unga kilo 250 mafuta ya kupikia mbuzi wawili na nguo za watoto na wanawake.

Baada ya kutoa msaada huo Jokate amesema kuwa ameguswa sana kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum ili nao washeherekee sikukuu ya Eid kwa furaha.

Kwa upande wake mkuu wa kituo hicho, Ahmed Shebe amemshukuru mwanamitindo huyo kwa msaada huo uku akiwahimiza wasanii wengine waige mfano Jokate.

Jokate kwsasa ni kaimu katibu mkuu wa uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *