Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo ametuliwa kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, amesema kuwa uteuzi huo wa Jokate ulifuata taratibu zote za chama.

Shaka amesema “Ni kweli amekaimishwa kwa kufuata taratibu zote za chama, kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilikutana Aprili 18, mwaka huu, Dar es Salaam na ndicho kimewakaimisha wakuu wa idara watano akiwamo Jokate.

Ameongeza kwa kusema  “Hao wanaolalamika hawajui kanuni na taratibu za jumuiya yetu, huwezi kupata nafasi kama kikao cha Kamati ya Utekelezaji hakijakaa,”.

Kwa upande wake, Jokate alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kuifanya jumuiya hiyo iwe karibu zaidi na vijana wa Kitanzania.

Jokate pia alikuwa miongozi mwa wanachama 450 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *