Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo amewataka watu kuacha kutumia lugha za matusi dhidi ya wanawake kwa kuwa wanawake ni watu wanaohifadhi maumivu na mambo mengi  kwenye moyo zaidi ya wanaume.

Jokate amesema mwanamke ni mtu ambaye anakumbana na mambo makubwa anayopaswa kukabiliana nayo mengine ni mazito lakini anayaweka moyoni mwake ili kufanikisha jambo hivyo anapaswa kuheshimiwa.

 Ameongeza kuwa yeye kwa upande wake mwanamke ni mtu mwenye moyo wa ziada ambaye hujitoa kwa ajili ya jamii lakini pia ni mchapa kazi na anajua kitu gani anataka.

Katika kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na EATV kuwachangia mabinti waende shule bila kukosa kwa kigezo cha kuepuka aibu inayosababishwa na ukosefu wa vifaa vya kujisitiri kipindi cha hedhi, Jokate amechangia kiasi cha shilingi laki moja.

Kampeni ya Namthamini imeanzishwa na EATV kwa ajili ya kuwasaidia watoto kike waweze kupata vifaa vya kujisitili wakati wakiwa katika hedhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *