Klabu ya Aston Villa wamemsajili aliyekuwa mchezaji wa Chelsea na nahodha wa timu ya Uingereza John Terry.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 36 ambaye mkataba wake na Chelsea umekwisha mnamo tarehe 30 mwezi Juni ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.

Terry alisema kuwa alikataa maombi ya kuendelea kucheza katika ligi ya Uingereza ili kujipatia fedha zaidi kwa sababu hakutaka kucheza dhidi ya Chelsea.

Aliichezea Uingereza mara 78, akaichezea Chelsea mara 717 na kuweza kushinda taji la 5 la ligi ya Uingereza mwezi Mei.

Villa ilimaliza ya 13 katika ligi ya daraja la kwanza msimu uliopita lakini kikosi hicho cha Steve Bruce ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upato kupanda na kucheza katika ligi ya Uingereza ya msimu wa 2017-18.

Meneja wa Birmingham Harry Rednapp alisema mnamo mwezi Juni kwamba klabu yake ilikuwa imemtumia ombi Terry ambaye alitangaza mnamo mwezi Aprili kwamba ataondoka Chelsea.

Terry amechezea Chelsea na Nottingham forest ambayo alicheza kwa mkopo 2000 kabla ya kutua kamili klabu ya Chelsea.

 

                         

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *