Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry amekanusha vikali madai kwamba Marekani ililipa kikombozi cha dola milioni moja kuwakomboa wafungwa wa taifa hilo waliozuiliwa nchini Iran.

Kerry amesema kwamba malipo hayo yalikuwa ya kutatua mgogoro kuhusu mpango wa ununuzi wa bidhaa za kijeshi.

Wanasiasa wa chama cha Republican wameishambulia serikali kutokana na malipo hayo.

Malipo hayo yalitolewa wakati wa kutia saini mkataba wa kinyuklia na ubadilishanaji wa wafungwa ambapo wafungwa wanne wa Marekani waliachiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *