Nyota wa mchezo wa mieleka nchini Marekani, John Cena na mpenzi wake Nikki Bella wametangaza kuwachana. 

Kwa mujibu wa mtandao wa US Weekly  umeripoti kuwa wawili hao wameachana na kufanya maamuzi hayo kuwa ya siri ili kuzingatia heshima ya kila mmoja.

Tetesi za wawili hao kuachana zilianza kusambaa mwezi uliopita lakini John Cena (40) alinukuliwa akisema kuwa hawaongozani pamoja kwa sababu ambazo alieleza kuwa angezitaja baadae.

Tujikumbushe tukio la John Cena alipomvisha pete mke wake Nikki Bella (32) ambaye naye ni mcheza mieleka mwaka jana Aprili 02.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *