Staa wa Bongo movie, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kwamba yeye ni mwanamke kamili na ameshakuwa kwa hiyo ana kiu ya kupata mume atakayemuoa ili kutimiza ndoto zake.

Staa huyo amesema “Mimi ni mwanamke kamili, nimeshakuwa sasa, kwahiyo kiukweli nina kiu ya mume kwani Mungu akinipa mume bora, nitaolewa”.

 

Johari: Baadhi ya filamu aliyoigiza kama anaolewa.
Johari: Baadhi ya filamu aliyoigiza kama anaolewa.

Vile vile muigizaji huyo amesema kwamba hataki kuzungumzia sana mambo yaliyopita, lakini muhimu kwasasa ni mume atakayemuoa kwani amechoka kukaa uhuni kama baadhi ya msataa wengine wa Bongo movie.

Johari ni muigizaji maarufu nchini ambapo amejizoelea sifa kupitia kazi zake tofauti alizowahi kuigiza vile vile muigizaji huyo ni mmoja wa waanzilishi wa RJ Company inayomilikiwa na yeye pamoja na Vincent Kigosi ‘Ray’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *