Waigizaji wakongwe wa Bongo Movie, Norah na Johari wamepata baada ya kumaliza bifu yao ya muda mrefu.

Chanzo cha bifu Lao ilikua ni mapenzi pamoja na shutuma za kurogana ambapo awali johari alikua mpenzi wa Ray kigosi baadae ilikuja kubainika nora nae anatoka kimapenzi na Ray.

Norah alipoulizwa kuhusu ugomvi wake na johari, alidai tu ni wivu wa kijinga na aligundua staa mwenzie huyo na ray wanamroga kufifisha nyota yake pamoja na kumuaribia madili ya filamu kwa baadhi ya ma producer nchini.

Hata hivyo sasa hivi wawili hao wanaonekana kupatana sana na kushirikiana kwenye baadhi ya mambo ya kijamii, pia tunategemea kuwaona pamoja wakiigiza kama ilivyokua awali, wote tunatambua umahiri wa johari na nora mbele ya camera,waswahili wanasema ,Old is Gold.

Baadhi ya movie za johari na nora zilizowahi kutikisa zamani ni JOHARI, DANGEROUS DESIRE,SIKITIKO LANGU na nyingine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *