Mchezaji wa Tenisi nambari moja kwa ubora nchini Uingereza, Johanna Konta ameifikia hatua ya tatu ya kombe la Rogers kwa kumfunga, Vania King kutoka nchini Marekani.

Johanna Konta  amefikia hatua hiyo kwa ushindi wa 7-5 6-1 dhidi ya mpinzani wake huyo kutoka nchini Marekani.

Mchezaji huyo ni namba moja kwa ubora nchini Uingereza lakini ubora wa Duniani yuko kwenye nafasi ya 14, katika hatua inayofuata atakutana na Mmarekani Varvara Lepchenko katika mashindano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *