Mkali wa hip hop Bongo, Joh Makini amesema kuwa yeye na kundi lake la Weusi hawashindani na msanii yoyote kwenye muziki nchini badala yake wanafanya kazi bora tu kwa mashabiki zao.

Joh Makini ambaye kwasasa anafanya vyema na ngoma yake ‘Waya’ amefunguka na kusema kuwa wao wamedhamiria kutoa muziki mzuri na si kushindana na mtu bali wanatimiza ndoto zao.

Mwanahip hop huyo amesema kuwa wao kama Weusi wanafanya muziki ili kutangaza nchi, kutimiza ndoto zao katika maisha na si kushindana na msanii yoyote yule.

 Mbali na hilo Joh Makini aliizungumzia ngoma mpya ya Fid Q ‘Kemosabe’ na kusema ni ngoma kali sana na yeye amependa jinsi ambavyo Fid Q amebadilika katika uimbaji kwani imekuwa tofauti na kazi zake nyingi za nyuma.

Joh Makini ni mwanamuziki kutokea pande za Arusha ambaye anaunda kundi la Weusi akiwa na wasanii wenzake kama vile Nikki wa Pili na G – Nakko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *