Mkali wa miondoko ya hip hop nchini, Joh Makini amefunguka na kusema kuwa katika vitu ambavyo hapendi kwenye kazi zake za kisanii ni kuwa na bifu na msanii mwenzake.

Joh Makini amesema kuwa  apendi kuwa na bifu na msanii yeyote kwasababu anaamini katika muziki wake na kuheshimu kila mmoja katika kazi yake.

Rapa huyo ameongeza kwa kusema kuwa katika mambo ambayo humuumiza sana ni kuona kazi za wasanii zikiwa zimezagaa mtaani na kuuzwa bila wasanii kunufaika na chochote.

Joh Makini amesema hayo kufuatia tetesi za mtaani kuwa ana bifu na mwanamuziki mwenzake Dully Sykes ambapo amesema habari hizo si za kweli kwasababu yeye hapendi bifu na wanamuziki wenzake.

Pamoja na hayo Makini amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwani kundi la weusi limejipanga vyema katika kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *