Mwanamuziki wa hip hop nchini kutoka Weusi, Joh Makini ameanza kutengeneza video mpya ya wimbo wake aliomshirikisha Davido kutoka Nageria.

Mipango ya kufanya nyimbo hiyo ilfanyika toka mwaka 2014 ambapo Davido alithibitisha colabo ya nyimbo hiyo alipokuja nchini kwa ajili ya Tamasha la Fiesta.

Kwasasa Joh Makini yupo na Davido nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushoot video ya wimbo huo ambapo haijajulikana lini itatoka rasmi audio pamoja na video yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Davido athibitisha ujio huo kwa kupost  picha akiwa pamoja na Joh Makini na kuandika maneno yalisomeka “Back to work On set shoot @johmakinitz ft Davido ….. TZ  x NAIJA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *