Mwanamuziki nyota wa hip hop nchini, Joh Makini amesema kuwa ile collabo yake pamoja na msanii Davido kutoka Nigeria inatarajia kuachiwa mwishoni wa mwaka huu.

Joh Makini amesema kuwa kama kila jambo litakwenda lilivyopangwa huenda mwishoni mwa mwaka huu akaachia kazi hiyo ambayo inasubiriwa sana na mashabiki wake.

 

Davido
Davido

Kwa upande mwingine msanii Joh Makini alisema collabo yake na msanii Bongo fleva Alikiba pia inakuja hivyo mashabiki wasitie shaka juu ya jambo hilo kwani lipo njiani kuja nalo.

 

Pia Joh Makini alisema kwa sasa lengo lake kubwa ni kuona anakuza muziki wa Hip Hop wa bongo Afrika na duniani kwa ujumla.

 

Joh Makini kwasasa anatamba na nyimbo yake inayokwenda kwa jina la Perfect Combo aliyemshirikisha mwanamuziki Chidnma kutoka Nigeria ambapo inafanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya TV na Radio vya ndani na nje ya nchi.

 

Mwanamuziki huyo ni mmoja wanounda kundi la Weusi ambapo linafanya vizuri pia, wasanii wengine wanaounda kundi hilo ni Nikki wa pili na G.Nako.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *