Mkali wa hip hop Bongo, Joh Makini amesema kuwa anajisikia furaha kuwa miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo za EATV mwaka huu kupitia ngoma yake ya Don Bother aliyomshirikisha A.K.A kutoka Afrika Kusini.

Ngoma hiyo imemuigiza Joh katika tuzo hizo kupitia vipenge viwili ambavyo ni Wimbo Bora wa Mwaka na Video Bora ya Mwaka.

Joh Makini amesema  amejisikia furaha na faraja kwa kiasi kikubwa kuona kazi yake inathaminiwa na kuingizwa katika tuzo hizo kubwa za muziki na filamu Afrika Mashariki.

Joh Makini amesema kuwa muziki huo ndiyo wenye nguvu zaidi kwa kuwa wasanii wake wengi ni wabunifu.

Tuzo za EATV zinatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mllimani City jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha wasanii wa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *