Joh Makini ashinda tuzo nchini Uganda

0
95

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joh Makini ameshinda tuzo nchini Uganda kupitia kipengele cha BEST COLLABORATION kupitia wimbo ‘Abaana Beeka’ alioshirikishwa na rapa Navio wa Uganda.

Joh Makini alikuwa anawania tuzo hizo kupitia kipengele vitatu ambavyo ni “Msanii Bora Mwaka” na wimbo wake wa Dangerous akishindana na wakali wengine kutoka afrika mashariki kama vile Khaligraph Jones King Kaka na Femi One.

Kipengele kingine alichowania Joh Makini ni Kolabo Bora ya Mwaka kupitia wimbo ‘Abaana Beeka’ alioshirikishwa na rapa Navio wa Uganda na ndio wameinuka washindi.

Kwa mwaka huu 2021 Joh Makini anakuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kuwani tuzo za nje ya nchi na kushinda mmoja ya tuzo hizo.

LEAVE A REPLY