Staa anayetamba na wimbo wa “Perfect Combo”, Joh Makini amesema anawaonea huruma sana watu wanaotumia muda wao kufanya vitu visivyokuwa vya msingi badala ya kufanya kazi.

Joh Makini amesema kauli hiyo baada ya wiki iliyopita mwanamuziki, Chid Benz kusema kwamba atishwi na Joh Makini na Ney wa Mitego kwasababu wanatengenezwa na media na hawawezi kufikia mafanikio kama aliyeyapata yeye katika muziki wa Hip-Hop.

Joh Makini amesema yeye haumizwi na kauli ya Chid Benz kwasababu kila mtu ana jinsi ya kuishi na mungu wake kwa hiyo hawezi kumjibu kutokana anapoteza muda wake kuongelea vitu visivyokuwa vya msingi.

Chid Benz alisema kwamba anaona Joh Makini na Ney wa Mitego wametengeneza kwa ajili ya kuja kushika game ya muziki wa Hip-Hip nchini lakini hakauna wanachokifanya na hawana nguvu ya kufanya hivyo.

Joh Makini kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ”Perfect Combo” aliyomshirikisha mwanamuziki Chidnma kutoka Nigeria kuku Chid Benz akitamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la “Chuma” aliyomshirikisha Raymond.

benz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *