Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Joh Makini ametoa pole kwa familia ya mwanamuziki wa Afrika Kusini, AKA baada ya kufariki kwa kupigwa risasi.

Joh Makini ambaye amewahi kufanya kazi na A.K.A kupitia wimbo Don’t Bother  Joh Makini amefunguka kwa urefu na kutoa pole kwa familia ya AKA pia nmna alivyofanikisha collabo yao.

Joh Makini ameeleza kusikitishwa na taarifa hizo huku akisema atumiss ukarimu wa AKA kwa alikuwa mtu poa sana, Joh Makini amefunguma kuwa hakutegemea kama AKA angekuwa mtu mkarimu sana kwa alivokuwa akimuona kabla ya kukutana Dar Es Salaam.

Pia ameongeza kuwa kitu ambacho hawezi kukisahau ni namna collabo yao ilivyofanikiwa na hata siku wanaingia studio AKA alianza kurekodi na Diamond ngoma yao ya MAKE ME SING lakini aliomba Joh Makini asubiri mpaka pale atakapomaliza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *