Golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Uingereza, Joe Hart leo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kujinga na klabu ya Torino ya nchini Italia kwa mkopo wa muda mrefu.

Kipa huyo amepoteza namba katika kikosi cha kwanza cha Manchester City chini ya kocha mpya Pep Guardiola.

Joe Hart hajaanza katika michezo mitatu iliyopita ya ligi kuu nchini Uingereza huku nafasi yake ikichukuliwa na kipa mkongwe Willy Caballero.

Manchester City wamemsajili golikipa Claudio Bravo toka Barca kwa mkataba wa miaka minne kwa ajili ya kuwa kipa namba moja katika klabu hiyo.

Pep Gurdiola ameonekana kutovutiwa na kiwango cha Joe Hart ambaye ndiyo namba moja katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *