Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amemtembelea na kumpa pole waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe baada ya kufiwa na mke wake juzi.

Kikwete amewasili msibani leo saa sita mchana na kuweka saini kwenye kitabu cha maombolezo.

Kikwete amemfariji Dk Mwakyembe na kumtaka awe mvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ambaye pia alimjulia hali Linah wakati akiwa hospitali.

Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda; Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji; Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi; Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga na viongozi wengine wa Serikali waliopo madarakani na wastaafu.

Mjumbe wa kamati ya mazishi, Andrew Magombano amesema mwili wa Linah utaagwa kesho baada ya ibada itakayofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kunduchi kuanzia saa nne asubuhi.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *