Raia wawili wa Morocco ambao walijaribu kuwaingiza wahamiaji katika eneo linalotawaliwa na Uhispania lililo kazkazini mwa Afrika la Cueta wakiwa wamejificha ndani ya gari na mwengine katika sanduku.

Wakati maafisa wa polisi wkikagua gari moja walikuta mtu mmoja akiwa amefichwa katika eneo la mbele la gari na mwengine amefichwa katika eneo la kiti cha nyuma cha gari.

Mwanamume huyo na mwanamke ,wanaodaiwa kuwa raia wa Guinea ,walipata huduma ya kwanza kwa kuwa walikuwa na hewa kidogo ya kupumua.

Kwengineko kijana mmoja wa asili ya Kiafrika alipatikana amefichwa katika sanduku la mwanamke.

Kisa hicho kilitokea mnamo mwezi Disemba 30 na mtu huyo anayeaminika kutoka Gabon alihitaji matibabu ya dharura.

Raia 50 wa Morocco na 5 wa Uhispania walijeruhiwa wakati wahamiaji 1,100 walipojaribu kupita ua huo na kuingia Cueta kutoka Morocco.

Hakuna aliyefanikiwa kupita ,lakini watu wawili walijeruhiwa walipokuwa wakivunja ua huo na kupelekwa hospitalini huko Ceuta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *