Klabu ya Manchester United imefungwa kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi cha wiki moja baada ya kufungwa 3-1 dhidi ya Watford kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.

Watford iliongoza baada ya Etienne capoue kufunga kutoka kwa krosi iliopigwa na Daryl Janmaat kabla ya Marcus Rashford kusawazisha.

Lakini mchezaji wa akiba Zuniga alifunga ikiwa imesalia dakika saba mchezo kukamilika.

Deeney baadaye alifunga penalti katika mda wa ziada baada ya Marouane Fellaini kuangushwa katika ebeo hatari.

Hii ni mara ya tatu mfulilozi kwa Manchester United kupoteza, ikishindwa 2-1 na Manchester City, baadaye ikapoteza 1-0 dhidi ya klabu ya feyenoord ya Uholanzi katikati ya wiki katika kombe la Europa ligi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *