Jiji la Paris la nchi Ufaransa na Los Angeles la nchini Marekani ndio majiji pekee yanayowania kuwa wenyeji wa michezo ya Olimpiki na Paralimpiki ya mwaka 2024.

Kumekuwepo na mapendekezo toka kamati ya kimataifa ya Olimpic kuyapa nafasi majiji yote mawili kwa michezo ya mwaka 2024 na ile ya 2028.

Paris wameiambia kamati ya michezo hiyo kuwa wao wanavutiwa na kuandaa michezo ya mwaka 2024 tu na sio ile ya 2028.

Ratiba ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki inaonyesha itatangaza mwenyeji wa michezo ya mwaka 2024 mwezi Septemba mwaka huu, huku majiji ya Lima, Peru, na Paris yakiwa na nafasi kubwa ya kushinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *