Jiji la Paris limechaguliwa  na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki mwaka 2024.

Jiji la Los Angeles nchini Marekani limeteuliwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka 2028.

Mwezi uliopita, kamati hiyo ilifanya maamuzi ya kuwa Olimpiki mbili za majira ya joto zitatolewa kwa wakati mmoja, baada ya miji kadhaa kuahirisha zabuni zao kutokana na wasiwasi wao kuhusu ukubwa, gharama, na utata wa kuandaa moja ya matukio makubwa kama hayo ya michezo duniani.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa uchaguzi wa mji wa Paris kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ni ishara kwamba ya kutambuliwa kwa mji na nchi kitu ambacho kila Mfaransa anapaswa kusherehekea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *