Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya Universe, Jihan Dimack amewasili katika mji wa Manilla nchini Ufilipino kwa ajili ya shindano hilo litakalofanyika Januari 30 mwaka huu.

Mashindano ya hayo ya urembo ya Universe ni ya 65 toka yaanze na mwaka huu yanatarajiwa kushirikisha nchini 80 kutoka duniani kote ambapo ni mrembo mmoja tu ndiyo atakayoibuka mshindi na kuchukua taji hilo.

Mshiriki huyo wa Tanzania, Jihan Dimack alikabidhiwa bendera ya taifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo ya urembo duniani ya Miss Universe.

Mwaka jana taji hilo la urembo la Universe lilikwenda kwa mrembo wa Ufilipino Pia Wurtzbach aliyeibuka mshindi baada ya kuwashinda warembo wenzake walioshiriki kwenye michuano hiyo ya urembo.

Tovuti hii inamtakia kila la heri mrembo huyo Jian Dimack ili aweze kuibuka mshindi kwenye shindano hilo na kuiwakilisha nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *