Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatia mbaroni watu watano wanaodaiwa kuvamia, kuvunja na kuiba pesa kwenye ofisi za Prime Attorneys.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa wamekamatwa kufuatia oparesheni kali mpaka kupatikana watuhumiwa hao.

Baada ya msako huo watuhumiwa walikamatwa na walipohojiwa, wote wamekiri kuhusika na tukio hilo huku wakitaja matukio mengine waliyohusika kupora.

Watuhumiwa hao ni; Said Idrisa Saleh (47), mkazi wa Mbezi Luis, Musatapha Ibrahim Said (35), mkazi wa Magomeni Mwembechai, Somfi Nguza Somfi (52), mkazi wa Magomeni Mapipa, Imani Mbago Mhina (36), mkazi wa Kimara Mwisho na Hussein Hajji Suleiman (45), mkazi wa Kigogo Mbuyuni.

Pia Kamanda Mambosasa amesema jeshi lake linaendelea na upelelezi kubaini watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.

Ofisi za kampuni hiyo zipo jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam jirani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *