Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limeendelea na mazoezi yake kwaajili ya ukakamavu ili kujiweka sawa na kupambana na tatizo la uhalifu.

Kamishna wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Simon Siro amewatoa hofu wananchi wasiwe na wasiwasi na zoezi hilo kwani halipo kwaajili ya kuwatisha bali lengo ni kupambana na wahalifu na majambazi nchini.

Aliongeza kwa kutoa mfano wa matukio yaliowahi kutokea kama panya road yanatokea sana maeneo ya Mbagala lakini wakaona kwanini wafanye mazoezi hayo kimya kimya ni vizuri wananchi wakaona jeshi lao pia wakaona ukakamavu wa askari.

Kwa upande mwingine kamishna wa oparesheni wa mafunzo ya jeshi la polisi, Nsato Nsazya aliwataka wananchi wasikejeli mazoezi hayo na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *