Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limethibitsiha kuwa aliyeuawa juzi na askari alikuwa ni mmoja wa majambazi na walitaka kuiba fedha sh. milioni 320 zilizokuwa zikipelekwa katika mashine ya ATM ya CRADB jengo la uhamiaji Kurasini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa kabla ya jambazi huyo kuuawa alitaka kumnyang’anya silaha askari Polisi ambaye alikuwa akisindikiza gari lenye fedha hizo.

Sirro amesema kuwa majambazi hao walikuwa na pikipiki mbili aina ya boxer na hawakujua kama gari lenye ela ni mali ya kampuni ya G4S lilikuwa likisindikizwa kwa nyuma ambapo lilikuwa linaendeshwa na Sophia Hussein.

Kamanda Sirro amesema kuwa jambazi huyo amefariki wakati akipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili lakini wamefanikiwa kupata simu yake na wenzake wanatafutwa na jeshi hilo.

Baada ya kusambaa taarifa za kifo cha jambazi huyo katika mitandao ya kijamii ndugu zake wamesema kuwa mtu huyo hakuwa akijihusisha na ujambazi lakini Sirro amesema waache uchunguzi uchukue nafasi yake.

Sirro amesema kuwa jesho la Polisi halitamfumbia macho mhalifu anayetaka kutumia silaha na ndugu wasitumie mwanya huo kuwalinda ndugu zao ambao ni wahalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *