Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limemkamata Askari Feki  anayefahamika kwa jina la Lyanga Baruti.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa mtuhumiwa huyo katika mahujiano alisema sare za jeshi hilo aliziiba kwa kaka yake na kizivaa.

Mtuhumiwa huyo amesema alizivaa na kwenda sehemu mbalimbali na kisha askari wakaweza kumnasa akiwa katika mizunguko yake.

Pia Kamanda Sirro amesema kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikiria  watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao walifanya matukio mawili tofauti ya uporaji katika maeneo ya Boko pamoja na Sinza jijini Dar es Salaam.

Kamishina Sirro amesema wakati polisi  wakiwa katika operesheni walifika maeneo hayo kisha majambazi wakaanza kutupa  risasi na polisi wakajibu na kuwapiga na wakaanguka ndipo waliweza kuwachukua kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili  ambapo walifariki wakiwa wanapatiwa matibabu.

Wakati huo huo jeshi la polisi limewakamta watu wawili ambao walikuwa wanazalisha Konyagi bandia ya chupa. Watuhumiwa hao ni Bahati Steve pamoja na Vumilia Andrea na uchunguzi unaendelea dhidi yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *