Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata silaha aina ya bunduki zikiwemo za kivita SMG sita ambazo zilikuwa zinamilikiwa kinyume na sheria katika wilya ya Ngorongoro mkoani humo.

Silaha hizo zimekamatwa kutokana na operesheni kufanya na jeshi la Polisi mkoani Arusha ili kukomesha matukio ya kihalifu yanayofanywa ndan ya mkoa huo.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kuwa baadhi ya silaha zilikuwa zimesalimishwa kwa viongozi wa kimila wa kimasai na wasonjo baada ya jeshi kutoa muda kwa wamiliki wa silaha kufanya hivyo.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa jeshi la polisi limeamua kuendesha operesheni hiyo baada ya kukithiri matukio ya kiharifu mkoani humo.

Kwa upande wao wananchi wameifia zoezi hilo huku wakilata jeshi la polisi kuwa karibu na wananchi ili kufanikiwa kwa kuwa wananchi ndiyo wanawajua wamiliki wa silaha haramu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *