Mahakama imetoa amri ya Jengo la Klabu ya Yanga lililopo mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam kupigwa mnada.

Jengo hilo linapigwa mnada kutokana na deni la kodi ya Majengo la Sh milioni 360 ambazo klabu hiyo inadaiwa na Serikali.

 Siku ya mnada imepangwa kuwa Agosti 19 yaani keshokutwa kuanzia saa 4 asubuhi na Msolopa Investment ndiyo itakayohusika na mnada huo.

Kampuni ya Msolopa kupitia kwa mkurugenzi wake, Ibrahim Msolopa, ilitangaza kuahirisha kwa mnada huo kutokana na makosa yaliyofanyika kabla ya kutoka kwa tangazo hilo.

Msolopa amesema kuwa walipanga mnada huo ufanyike leo na sio Jumamosi kama ambavyo tangazo linavyosomeka magazetini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *