Staa wa Bongo Movie, Jacob Stephen ‘JB’ amesema kuwa hawalaumu wasanii ambao wamekuwa wakiendesha maisha yao ya sanaa kwa kutafuta ‘kiki’ au kufanya skendo ili wapate umaarufu.

Amesema kwa upande wake hawezi kufanya hivyo kwani anaamini kuwa maisha ya skendo huwafanya wasanii waonekane wahuni washindwe kuaminiwa na kudharauliwa na baadhi ya watu.

JB alisema kwamba amekuwa akiaminiwa sana kwenye kazi yake hiyo ya sanaa kutokana na kuwa na nidhamu na kuziepuka skendo siziso na msingi ili kutunza kipaji chake.

JB: Akiwa na rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete
JB: Akiwa na rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete

Staa huyo ameendelea kusema kwa mfano akienda kuomba location sehemu yoyote baba mwenye nyumba na mke wake mpaka watoto wote wanajua wapo salama kutokana na kuwa na nidhamu.

Mbali na hilo JB amedai tabia yake hiyo imemfanya kuaminiwa hata na makampuni makubwa kwani wanaona kuwa huyu mtu ni mtu sahihi si mtu ambaye wanaweza kusikia amefumaniwa na kutimuliwa na mapanga huko bali wanakuwa na imani kuwa atafanya vyema katika jukumu atakalopewa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *