Staa wa Bongo movie, Jacob Steven ‘JB’ ameshiriki katika igizo la “Kumekucha” ambalo limeandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujishughulisha na kilimo kutokana na uhaba wa soko la ajira nchini kwasasa.

Katika igizo hilo, JB ametumia jina la “Mzee Kidevu” ambaye shughulii yake ni kununua mazao kwa wakulima kwa bei ya chini na ya ukandamizaji na kuwafanya wakulima hao kuendelea kuwa na maisha duni huku yeye akijinufaisha zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi wa igizo hilo, JB amesema amefurahi sana kushiriki katika igizo hilo ambalo linafundisha na kuhamasisha vijana kujihusisha zaidi na masuala ya kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini kama suluhisho la kupata ajira.

Staa huyo amesema kushiriki kwake katika igizo hilo umempa mwanga mkubwa na kupanua wigo wa kazi zake za uigizaji.

JB ameongeza kwa kusema kabla ya kuingia kwenye kuigiza, alikuwa mnunuzi wa mazao hasa mahindi kule Kibaigwa mkoani Dodoma na kusaga na kuuza unga wa chakula

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *