Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu staa wa Bongo movie, Jacob Stephen ‘JB’ anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la “Kalambati Lobo” itakayotoka mwezi Agosti mwaka huu.

Staa huyo amesema filamu hiyo imetengenezwa chini ya kampuni yake ya Jerusalem Films Company imewakutanisha baadhi ya wasanii kama Diana Kimaro alioigiza kwenye filamu ya Danija ambayo pia iliandaliwa chini ya kampuni hiyo.

JB kupitia ukarasa wake wa Instagram amesema walikaa kimya sana toka mwaka huu uanze baada ya kutoa filamu ya ‘Chungu cha tatu’ ambayo ilitoka mwishoni mwa mwaka jana kwa hiyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea filamu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *