Muigizaji wa Bongo Movie, Jacob Stephen  (JB) amesema kuwa kutopata mtoto kwake hakujaaribu ndoa yake.

JB amesema kuwa hajabahatika kupata mtoto kwenye ndoa yake lakini bado hajakata tamaa na anaamini ipo siku Mungu atajibu maombi yake.

Muigizaji huyo amekiri kukaribia kufikisha umri wa miaka 50 amewataka watu wote ambao hawajajaliwa kupata watoto wasiache kumshukuru Mungu na siku zote waishi maisha ya furaha.

JB amesema kuwa hawezi kumsaliti mke wake kwa kuwa na wanawake wengine kwa sababu kufanya hivyo ni kujiunganisha kiroho na watu tofauti tofauti kupitia mapenzi.

Katika hatua nyingine msanii huyo amesema kuwa hapendi siasa na hata siku ikitokea akapatiwa nafasi ya uongozi hataweza kufanya kwa kuwa maisha yake kitu kinachompatia furaha ni uigizaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *