Rapa mkongwe wa Marekani, Jay Z ameanza kujaribu kupata haki miliki ya nyimbo za mwanamuziki marehemu Prince.

Jay Z amekutana na mmoja wa ndugu wa Prince, Tyka na kumueleza kuwa yupo tayari kununua haki miliki za nyimbo za Prince ambazo bado hazijatoka kwa kulipa kiasi cha dola milioni 40.

Prince
Prince

Hata hivyo Tyka hana haki ya kusaini mkataba huo mpaka pale atakapokutana na meneja wa marehemu Prince na baadhi ya ndugu zake wengine wenye haki na nyimbo hizo.

Kabla ya kifo chake, Prince aliwahi kuachia nyimbo zake kwenye mtandao wa Tidal lakini pia wawili hao walikuwa na urafiki wa ukaribu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *