Rapa mkongwe nchini, Jay Moe amesema kuwa Juma Nature amefanya mambo makubwa sana mpaka muziki kufikia hapa ulipo.

Jay Moe ameongeza kwa kusema kuwa alichokifanya Juma Nature kwenye game ya bongo fleva ni kitu cha kuthaminiwa sana kwani ameleta mchango mkubwa kwenye muziki huo mpaka kufikia hapa.

Rapa huyo mkongwe aliyewahi kutamba na wimbo ‘Kimya Kimya’ amesema kuwa wataendelea kumheshimu Juma Nature kwani vitu ambavyo amevifanya, ndivyo vimesababisha wasanii kama kina Diamond kujulikana kimataifa.

Juma Nature
Juma Nature

Jay Moe amesema kutokana na aina hiyo ya muziki wa Juma Nature, ndiyo umewafanya vijana wengi na kufuata nyayo zake, ikiwemo yeye mwenyewe na kuandika mistari ya wimbo wa stori 3 na Jua na mvua.

Pongezi hizo za Jay Moe zimekuja baada ya Juma Nature kusheherekea siki yake ya kuzaliwa hapo jana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *