Winga wa Ubelgiji, Adnan Januzaj ameifungia timu ya Sunderland bao lake la kwanza baada ya kuifunga Shrewsbury 1-0 kwenye mechi ya raundi ya pili ya Kombe la Ligi nchini Uingereza.

Goli hilo limemsaidia meneja wa timu hiyo David Moyes kupata ushindi wake wa  kwanza tangu achukue nafasi iliyoachwa wazi wa Sam Allardyce aliyeichukua timu ya taifa ya Uingereza.

David Moyes: Akishngilia ushindi kwenye mechi ya kombe la ligi nhini Uingereza.
David Moyes

Kiungo wa kati wa Sunderland, Steven Pienaar alipoteza nafasi nzuri ya kufunga katika kipindi cha kwanza huku mshambuliaji Joel Asoro nae akishambulia lango la Shrewsbury mara mbili.

Baada ya mechi hiyo klabu ya Sunderland imethibitisha kwamba beki wa Atletico Madrid, Javier Manquillo amepimwa vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya msimu wa Ligi kuu nchini Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *