Tetesi zilizoenea katika mitandao nchini Marekani zinasema kuwa mwanamuziki mkongwe wa Marekani, Janet Jackson atampa mtoto wake jina la kaka yake mkali wa Pop dunia, Michael Jackson.

Kutokana na taarifa hiyo jina la mkali huyo wa pop Michael Jackson litaendelea kuishi kwenye midomo na mawazo ya watu baada ya Janet kuamua kutoa jina hilo.

Mitandao hiyo imeripoti kuwa jina la mtoto wa Janet litafanana na jina la Michael Jackson kama kumbu kumbu ya marehemu kaka yake.

Mwanamuziki huyo na mume wake Wissam Al Mana tayari wanachumba kimetayarishwa kwaajili ya mtoto huyo atakayezaliwa.

Pamekuwa na tetesi kuwa Janet atajifungua kwa shida kutokana na umri wake ila zimekuwa zikizimwa na kauli za madaktari wake wanaosema anaendelea vizuri tu.

Janet Jackson na mumewe ambaye ni rais wa kiarabu wanatarajia kupata mtoto wa kiume baada ya Janet kubeba ujauzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *