Mwanamuziki nyota wa Marekani, Janet Jackson amethibitisha rasmi kwamba anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50.

Janet amesema kuwa anashukuru Mungu kwa baraka aliyonayo huku akapigwa picha na tumbo lake linalozidi kuwa kubwa kudhihirisha uja uzito.

Fununu kuhusu uja uzito wake zilizuka Aprili alipojitokeza kuahirisha shughuli zake na tamasha la kimataifa ‘Unbreakable’ akisema anataka kupanga uzazi na mumewe Wissam al-Mana.

Ameonekana hivi karibuni London akinunua vitu katika duka la watoto.

Jarida la The People limenukuu duru iliyo karibu na familia ya Jackson aliyesema: “Ana furaha sana kuhusu uja uzito wake na anedelea vizuri sana. Ana raha kuhusu kila kitu.”

Katika video iliowekwa kwenye Twitter mwezi April, amewaambia mashabiki wake kuwa ana ahirisha shughuli zake, kwasababu “kumekuwa na mabadiliko ya ghafla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *