Baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Stoke City, mshambuliaji wa timu ya Leicester City, Jamie Vardy atakosa michezo mitatu ya ligi hiyo.

Mshambuliaji huyo alitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Stoke City, Mame Diouf.

Kutokana na kosa hilo mchezaji huyo amefungiwa kutocheza michezo mitatu ya ligi kuu nchini Uingereza ambayo ni dhidi ya Everton kwenye uwanja wa Goodson Park dhidi ya West Ham utaochezwa uwanja wa King Power.

Mchezo mwingine atakaokosa mshambuliaji huyo ni dhidi ya Middlesbrough Januari 2 mwakani.

Vardy anatarajia kurejea uwanjani kwenye mechi ya kombe la FA dhidi ya Everton ifikapo Januari 7 mwakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *