Kupitia video yake aliyoiweka Instagram na kutangaza kuwa mwaka 2017 utakuwa na mambo makubwa zaidi, hatimaye Diamond Platnumz ameanza kuyaweka wazi mambo hayo.

Unaikumbuka track yake aliyofanya na staa wa Marekani, Ne-Yo, MARRY YOU?

Ukiwa umepita muda mrefu tangu kurekodiwa kwa ngoma hiyo huku promotion yake ikitaja maeneo itakapokuwa ikichezwa ikiwemo Marekani na barani Ulaya, sasa video ya ngoma hiyo kuanza kuwika Afrika.

Kituo cha Trace TV cha Afrika Kusini kimetajwa kuwa kituo cha kwanza ambacho kitaicheza video ya ngoma hiyo.

Ngoma hiyo inatarajiwa kuchezwa kwa mara ya kwanza siku ya leo.

 

Ingawa watu wengi wameuona wimbo huo kupitia YouTube lakini mashabiki wanaotumia zaidi Luninga kutazama kazi za wasanii wawapendao, walikuwa hawajabahatika kuwaona Platnumz na Ne-Yo wakiperform Marry You.

Cheki ngoma hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *