Aliyekuwa mpiga tarumbeta katika bendi ya mwanamuziki wa rege nchini Jamaica, Bob Marley aitwae Headley Bennett amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85.

Headley Bannett alishiriki katika wimbo wa kwanza wa Bob Marley uliokuwa unaitwa ‘Judge Not miaka ya themanini.

Kifo cha mpiga tarumbeta huyo kimethibitishwa na mwanawe Carol Bennett hapo jana,

Headley Bennett: Akipiga tarumbeta kwenye bendi ya Bob Marley enzi za uhai wake.
Headley Bennett: Akipiga tarumbeta kwenye bendi ya Bob Marley enzi za uhai wake.

Carol hakusema sababu maalum ya kifo cha mwanamuziki huyo lakini alisema babake alikuwa akiugua shinikizo la damu .

Pia Benneth aliwahi kushiriki na wanamuziki wa nyimbo za rege kama vile Bunny Wailer na Gregory Isaacs.

Vile vile alipewa heshima na serikali ya Jamaica mwaka wa 2005 kama Mjamaica wa sita mwenye hadhi ya juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *